Get Mystery Box with random crypto!

... Safari ya wapinzani wa Yanga Marumo Gallants hadi nusu | OFFICIAL YANGA FORUM 🇹🇿

... Safari ya wapinzani wa Yanga Marumo Gallants hadi nusu fainali.

» Gallants walifuzu kucheza michuano ya CAFCC baada ya klabu ya Mamelodi Sundowns kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu na michuano ya super 8 (FA)...

... Hivyo kikanuni ikabidi Gallants waende CAFCC kwa sababu walicheza fainali na Mamelodi licha ya kupoteza.

» Hawafanyi vizuri kwenye ligi kuu lakini hawatabiriki, wanawachezaji wazuri lakini upepo mbaya kwenye ligi kuu umewapenda. Wanashika nafasi ya (14) kati ya timu (16).

Pia wanatumia vizuri uwanja wao wa nyumbani japo hawana mashabiki wengi.

Play off - CAFCC
Al Ahli Tripoli 1 - 0 Gallants
Gallants 3 - 0 Al Ahli Tripoli

Group stage - CAFCC
Gallants 4 - 1 Al Akhdar
Lupopo 1 - 2 Gallants
USM Alger 2 - 0 Gallants
Gallants 2 - 0 USM Alger
Al Akhdar 4 - 1 Gallants
Gallants 3 - 2 Lupopo

04 - Kushinda
02 - Kupoteza

» Hawana tofauti kubwa na Yanga kwenye group stage, Yanga yeye alishinda (4) akasare (1) na akapoteza (1).

Quarter final - CAFCC
Pyramids 1 - 1 Gallants
Gallants 1 - 0 Pyramids

Semi final - CAFCC
Yanga ? - ? Gallants
Gallants ? - ? Yanga

NB ; Sio timu tishio wala sio nyepesi.. Yanga wakijipanga vizuri fainali ileeee ...

... Kwa sababu
Hata Rivers walikuwa na rekodi nzuri kama hii nyumbani kwao, Yanga ndio walioenda kuiharibu, Rivers walikuwa wana mwaka 1 hawajapoteza mechi nyumbani kwao tena wakizifunga timu kubwa tu Africa.